Quantcast
Channel: TEAMTZ
Viewing all 2148 articles
Browse latest View live

PICHA:Licha ya kuwa na michoro ya ‘tattoo’zaidi ya 14,Chris Brown achora ‘tattoo’ ya sura ya mwanae Royality.

$
0
0

Chris Brown ambae alichora tattoo ya kwanza  akiwa na umri wa miaka 13,tayari ana michoro tofauti zaidi ya kumi na nne kwenye mwili wake,michoro iliyochorwa kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake kama kifuani,mikononi,mgongoni na shingoni huku ikiwa na maana tofauti.

LAS VEGAS, NV - JANUARY 01:  Singer Chris Brown performs at Drai's Beach Club - Nightclub at the Cromwell Las Vegas kicking off Drai's LIVE 2016 on January 1, 2016 in Las Vegas, Nevada.  (Photo by Bryan Steffy/Getty Images for Drai's Beachclub-Nightclub)Kupitia ukurasa wake wa instagram staa huyo wa single ya “Back to sleep”ali-post picha inayoonyesha mchoro wa sura ya mwanae Royality na kuandika…. ‘I do what the f*** I want.’

tattooooo breezy 009

breeeeeeezyyyyy tatooo

breeeeezy royality 001                                                 Royality.

Royality ni binti na mtoto pekee wa Chris Brown aliezaa na mwanamke anaefahamika kama Nia Guzman,kitendo kilichopelekea Mwanamuziki huyo kutengana na aliekua mpenzi wake ambae pia ni mwanamitindo Karruche Tran mapema mwaka jana,baada ya mwanamitindo huyo kubaini kuwa Chris Brown ni baba wa mtoto huyo.

Hata hivyo mapenzi ya Mwanamuziki huyu kwa mtoto wake hayajaanzia kwenye mchoro huu wa ‘tattoo’ kwani mwezi August 2015,Breezy alitangaza kuachia album yake mpya aliyoipa jina la mwanae “Royality”ambapo kwenye artwork-cover ya album hiyo,ilimuonesha Chris Brown akiwa amembeba mwanae.

chris-brown-royalty-coverHata hivyo miezi ya hivi karibuni kumekua na mgogoro kati ya Chris Brown na Mama wa mtoto huyo,mara baada ya mwanamke huyo kumfikisha mahakamani akipinga mwanamuziki huyo kumlea binti yao kwa madai kuwa Brown amekua akijihusisha na vurugu na matumizi ya madawa ya kulevya kama ‘bangi’,ambapo mahakama ilitupilia mbali madai hayo na kumpa Chris Brown uhuru wa kukaa na binti yake kwa siku 12 kila mwezi,na kutakiwa kumlipa Mama wa mtoto huyo kiasi cha dola $2,500 kila mwezi kama malipo ya malezi (child support allowance),huku jina la binti huyo likibaki kuwa Royality Brown.

 


Angel Di Maria aingoza Argentina kuiadhibu Chile kwenye mchezo wa kwanza wa michuano ya Copa America.

$
0
0

Argentina wameinyuka Chile mabao 2-1 katika mchezo wao wa kwanza wa kundi D kwenye michuano ya Copa America mchezo uuliochezwa katika uwanja wa Levi huko Clara, Calif.

Di Maria-Argentina

Argentina maarufu kwa jina la ‘La Albiceleste’ walikuwa bila ya nyota wao Lionel Messi kutokana kuendelea kuuguza majeraha yake ya mgongo aliyopata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Honduras uliochezwa Mei 27 ambapo licha ya  kutoanza vizuri dakika za kwanza za mchezo,Argentina walibadilika na kucheza kwa kasi ya aina yake na mnamo dakika ya 51, Angel Di Maria alifunga goli maridhawa baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Eva Banega.

Baadaye Argentina waliongeza bao la pili dakika ya 59 lililofungwa na Eva Banega baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Angel Di Maria huku bao pekee la Chile lilifungwa kwa kichwa na Jose Fuenzalida dakika ya 90 kutokana na pasi nzuri ya Fabian Orellana na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Kwa sasa Argentina na Panama wanaoongoza kundi D wote wakiwa na alama tatu na magoli mawili ya kufungwa na moja la kufungwa huku Chile na Bolivia wakiwa hawana pointi na wamefungwa magoli mawili  kila mmoja na kufunga goli moja.

Timu zote zitarudi kundini June 10 ambapo Chile watakuwa na kibarua dhidi ya Bolivia huku Argentina wakiwakabili Panama.

Dondoo muhimu kuhusu mchezo huo:

  • Bila ya Messi, hakuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji ya Argetina kwani licha ya Lionel Messi kutocheza mchezo wa jana baada ya kuwa na majeraha yake ya mgongo,kazi ya Banega na Di Maria iliwasahaulisha Argentina juu ya Messi.
  • Di Maria afunga goli na kuli-dedicate kwa bibi yake,ambapo mara baada kufunga goli hilo,alinyanyua T-shirt ambayo ilikuwa na ujumbe ulioandikwa kwa mkono,ujumbe uliokuwa maalum kwa bibi yake aliyefariki hivi karibuni.Baada ya mchezo huo, Di Maria ambaye alikuwa akitokwa machozi na alisema kwamba, bibi yake alikuwa ndiyo kila kitu kwake.
  • Argentina na Chile walikutana katika fainali ya michuano hii mwaka jana na Chile kuibuka na ushindi wa matuta. Sanchez.

Mchezaji na Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria,Stephen Keshi afariki dunia.

$
0
0

Tasnia ya michezo nchini Nigeria imepata pigo baada ya taarifa za kifo cha kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Okechukwu Keshi aliefariki ghafla mapema leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 54.

 

Mchezaji huyo wa zamani  ambaye pia mwaka jana alimpoteza mkewe Kate Stephen Kesh,aliyekuwa na umri wa miaka 33, kwa ugonjwa wa kansa, inaarifiwa kifo chake  kimetokana  na matatizo ya moyo yaliyokua yakimkabili ambapo kwa mujibu wa wanafamilia na marafiki wa karibu wa mkongwe huyo wa soka,wamedai kuwa licha ya matatizo ya moyo yaliyokua yakimkabili,Keshi hakuonesha dalili zozote za kuumwa mpaka mauti yanamfika.

JONATHAN AND KESH 00006Rais msataafu wa Nigeria Godluck Jonathan (L)akimkabidhi Stephen Keshi cheti cha heshima baada ya kuingoza Nigeria kutwaa kombe la mataifa ya Afrikka  mwaka 2013.

Mwaka 2013 Keshi aliweka rekodi baada ya kuipa Nigeria kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa kocha pekee mzawa kufanya hivyo na kushilikilia rekodi ya kuwa kocha wa pili kushinda kombe hilo akiwa kama mchezaji na baadaye kocha rekodi ambayo awali iliwekwa na Mahmoud El-Gohary wa Misri.

Akiwa kama mchezaji  Stephen Keshi aliiwakilisha  Nigeria kuanzia mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 20, mpaka mwaka 1994 mwaka ambao Nigeria waliibuka mabigwa wa kombe la mataifa ya Afrika na kufika hatua ya robo fainali ya kombe la dunia ambapo  mara nyingi aliitumikia Nigeria kama nahodha na kufunga magoli muhimu hasa ukizingatia nafasi yake aliyokuwa akicheza, kama beki wa kati.

Akiwa kama Kocha,mbali na kjifundisha timu ya taifa ya Nigeria,Keshi amewahi kuzifundisha timu za taifa za Togo na  Mali huku akiiongoza Nigeria kwenye michuano ya kombe la dunia mnamo mwaka 2014 nchini Brazil.

Huu ndo ukweli kuhusu Dili kati ya Rock Nation ya Jay Z na Tiwa Savage.

$
0
0

Afro-Pop hit maker Tiwa Savage na Meneja wake ambae pia ni mmiliki wa music label ya Mavin Music Don Jazzy hatimae wamesaini mkataba na music label ya Roc Nation inayomilikiwa na Hip-Hop Legend Jay Z mara baada ya wanamuziki hao kukutana kwenye ofisi za makao makuu ya Rock Nation jijini New York nchini Marekani.

mavin and rock nation 0001Dili hiyo kati ya Tiwa Savage anaefanya vizuri na hit song yake ya “If I Start To Talk”,imefanikishwa na binamu wa Jay Z anaefahamika kama Brian “Bee-Biggs”ambae mwaka jana alizuru nchini Nigeria na kufika kwenye makao makuu ya music label ya Mavin Music jijini Lgos nchini Nigeria ambapo licha kusaniwa na Rock Nation,bado Tiwa Savage atabaki kuwa chini ya Mavin Music inayomilikiwa na Don Jazzy huku Rock Nation wakihusika na shughuli za uzambazaji na kumtangaza msanii msanii huyo kimataifa.

mavin and rock nation 0002                               Bee-Biggs(L),Tiwa Savage(C) na Don Jazzy.

Ikumbukwe kuwa Rock Nation inayomilikiwa na Jay Z,inawasimamia baadhi ya wanamuziki wakubwa duniani kama Rihanna,Jay Cole,Rita Ora na Shakira na kumfanya Tiwa Savage kuwa msanii wa kwanza kutoka barani Afrika kusaniwa na label hiyo kubwa ya muziki duniani.

 

Picha: Rae Sremmurd wakava jarida la The Fader, wazungumzia kumuandikia Beyonce wimbo wa Formation

$
0
0

Wasanii wa kundi la ‘Rae Sremmurd’ Swae Lee na Slim Jxmmi wamekava toleo jipya la jarida la ‘The Fader’

rae-sremmurd-the-fader

Swae Lee amefunguka kuhusiana na kuandikia baadhi ya vipande kwenye wimbo wa Beyonce ‘Formation’

df

“Wakati naandika kipande cha Formation ya Beyoncé  sikufikilia chochote kama atauchukua Beyonce, ” alisema. “Huwa naandika nyimbo nyingi, hivyo nilikuwa naandika kama wimbo mwingine tu. miezi michache baadaye , Mike [WiLL Made-It]  akaniambia kwamba Beyoncé anautaka. Sikuamini!”

cx

Aliongeza kuwa alishangazwa na jinsi Beyonce alivyoongeza utaalamu wake kwenye wimbo huo, Soma Interview yao nzima Hapa

F104_FEATURE_SREMM_gavillet_04_web_odz4uw

 

F104_FEATURE_SREMM_gavillet_18_web_ubpd7e

F104_FEATURE_SREMM_gavillet_02_web_i1i4su

F104_FEATURE_SREMM_gavillet_06_web_vakmbx

 

Video: Wiz khalifa na Amber rose wakamilisha talaka yao, waenda kusherekea pamoja ‘Strip club’

$
0
0

Wiz khalifa na Amber rose ni watu watofauti, huku mastaa wengi wakiwa wanaachana na na bifu nzito lakini sio wanandoa wa zamani na wazazi, Wiz khalifa na Amber rose.

Talaka ya ndoa ya Wiz khalifa na Amber rose imekamilika jumatatu hii na wanandoa hao wa zamani waliamua kwenda kusherekea pamoja kwenye ‘Strip club’ ya Ace of Diamonds, huko Los Angeles.

Kwa mujibu wa TMZ, Wiz Khalifa anatakiwa amlipe Amber rose dola 644,000 nusu ya dolla Million 1 ya talaka ya ndoa hiyo, nusu nyingine ashalipa pia atatakiwa atoe dola 14,800 sawa na Million 32.4 za Kitanzania kila mwezi kwa ajili ya malezi ya mtoto wao, Sebastian. Wote wana haki sawa ya malezi.

Wapenzi hao wa zamani wameonekana kupeana support na kuwa karibu hata baada ya kuachana, Wiz khalifa amepanga kutokea kwenye show ya Amber rose ‘Amber talk show’.

Promota wa Nigeria aishitaki Roc Nation na Rihanna kwa kutotokea kwenye show iliyotakiwa kufanyika mwaka 2013

$
0
0

Roc Nation na Rihanna wamefikishwa kortini na muandaji wa matamasha wa Nigeria aliyewashitaki kwa kutotokea kwenye show iliyotakiwa ifanyike mwaka 2013 japo aliwalipa.

Promota huyo anayejulikana kwa jina la Chris Ubosi, amembuluza muimbaji huyo wa ‘Work’na label yake Kortin kwa madai ya kuwa alilipa Dola 425,000 kwa ajili ya show hiyo ambayo Rihanna alitakiwa atumbuize kwa dakika 65 tu lakini hakutokea.

maxresdefault (2)

Promota huyo amedai kuwa aliongea na wawakilishi wawili wa Rihanna,na lebel yake ya Roc Nation inayomilikiwa na Jay Z na kuwalipa kiasi icho cha pesa, amesema show hiyo iliyotakiwa ifanyike May ilisogezwa hadi Julai baada ya wawakilishi hao kuomba asogeze mbele lakini cha ajabu hakuna aliyetokea hadi leo.

Ubosi anataka kulipwa Dola laki 1.6, Hata hivyo Roc Nation imekanusha kufanya mzungumzo yoyote na Promota huyo.

 

PICHA:One Love Record ya Tiddy Hotter kumtambulisha msanii mpya weekend hii.

$
0
0

Record label mpya inayofahamika kama ‘One Love Record’ chini ya producer Tiddy Hotter inatarajiwa kumtambulisha msanii mpya wekeend hii ikiwa ni pamoja na ku-release kazi ya kwaza ya msanii huyo ambayo imeandaliwa kwenye studio za ‘One Love Record’ na producer Tiddy Hotter.

Akizungumza na Teamtz.com Tiddy Hotter ambae amefanya kazi na wasanii  kama Ben Pol,Belle9,Godzila,G-Nako,Fid-Q na Stamina amedai kuwa awali alikua akifanya shughuli zake za kimuziki mkoani Mwanza ila ameamua kuhamishia makazi yake Dar es salaam na kufungua studio yake iliyopo maeneo ya Survey-Makongo juu na kuongeza kuwa mpaka sasa ameshafanya kazi na wanamuziki wakubwa nchini ila kwa mara ya kwanza amekusudia kumtambulisha msanii mpya ikiwa ni pamoja na nyimbo yake ambayo itakua kazi ya kwanza kutoka kwenye record label hiyo anayoimiliki.

TIDDY HOTTER NA SOUDY BROWN 001        Tiddy Hotter(r)akiwa na  Co-Host na Producer wa kipindi cha XXL cha Clouds Fm,Soudy Brown.

“nimefanya kazi na wanamuziki wakubwa wengi tu tangu nifungue studio yangu mpya ila siwezi kuwataja kwa sasa coz plan yangu kwanza ni kuleta vipaji vipya kwenye muziki wetu wa kitanzania ….as to prove that nimeamua kuanza na Mdadisi,watu wengi hawamfahamu ila trust me kuna kitu kwa huyu jamaa na naamini watu watafurahia kazi hii ambayo nimeianda kwa mikono yangu….nyimbo yake itatoka rasmi tarehe 11-06-2016,i mean jumamosi hii na itapatikana mtandaoni pia”.Alidai Tiddy Hotter.

TIDDYHOTTER NA BELLE 9                                       Tiddy Hotter & Belle9 @One Love Record.

MDADISI                                                                 Mdadisi.

 

BEN PAUL ON MDADISI 02

BARAKA DA PRINCE ON MDADISI 001Ikumbukwe kuwa Tiddy Hotter ndie alietengeneza hits kama “Burger,Movie & Selfie” ya Belle9,na “Nisome” ya Godzila na G-Nako.

 


Ulikuwa unafahamu kama wivu ni ugonjwa wa kisaikolojia?

$
0
0

Wazee wa zamani wana msemo unasema wivu kidonda , sio uongo kuwa na wivu si jambo baya sana  ila wivu uliopitiliza ni ugonjwa, na wivu husababishwa na wasiwasi wa kumpoteza ulie nae kwa mtu mwingine, hii inafanya mtu kutokuwa na imani na mpenzi wake hata kama akitoka kwa dakika chache tu.

Nasema wivu ni ugonjwa kwa nini, wivu unaweza sababisha ugomvi, wivu unaweza leta maumivu kwako au hata kwa mpenzi wako, ndugu jamaa na marafiki wivu unaleta chuki na hata wengine kuchukia mapenzi nakuamua kuwa pekeyao, tayari inaleta matatizo ya kisaikolojia

Nini Ufanye kuzuia wivu uliopitiliza

  1. Mwamini mwenza wako

amini

Inawezekana ikawa ni kazi ngumu kidogo lakini, hakuna dawa nzuri ya wivu kama kuamini mpenzi wako ni muaminifu na hawezi kukusaliti hata kama unajua ni ngumu kujipa moyo jua ya swala hilo.

 

  1. Acha kujifananisha na wengine

Usijaribu kujifananisha na wengine, wakati mwingine wivu pia unaanzia kwa mtu mwenyewe kutojiamini sababu anajiona havutii kama wanawake/wanaume  wengine na pengine anashangaa kwanini mwanaume Yule au mwanamke Yule kamchagua kwahiyo anakuwa na hofu ipo siku mtu Yule atakwenda kwa mtu aliekuwa na mvuto zaidi yake au anaependeza zaidi yake, kwahiyo ni vyema ukajikubali na kuto jifananisha na wengine.

 

  1. Jiandae Kuishi Maisha Bila Mpenzi Wako

woman-showing-jealous-friend-engagement-ring

Ndio, najua inaonekana kama ujinga hivi ila sio ukiwa na wivu mara nyingi kitu kinachokuja kichwani ni uoga na unawaza utaishi vipi bila ya mtu Yule, sasa ni vizuri ukawa huru sababu siku akiondoka mtu Yule unaweza changanyikiwa,

Wivu unaondoa mapenzi na unaleta chuki  hasira, na mapenzi yanahitaji zaidi uhuru wa nafsi usiwe na uoga wa kumpoteza mtu Yule kwa sababu tu unahisi akiondoka utakufa, jiandae kisaikologia hii itakusaidia kuishi kwa amani kwani hutokuwa na wasiwasi na itapunguza wivu.

  1. Usimfanyie Mtu  Makusudi

Kuna wakati watu wanafanya michezo na mioyo ya watu kumtia mtu wivu makusudi ili aone atafanyaje, usicheze hiyo michezo hii inaonyesha hujiamini kwa mpenzi wako au kwasababu umeona anaongea na mtu na haujapenda sio lazima na wewe umtie wivu siku nyingine na mtu mwingine.

 

  1. Acha Kuwaza Vitu ambavyo Havipo

Man trying to comfort his grumpy wife

Tunaita “Imagination”  watu huwaza sana na kupata picha zao wenyewe kichwani ambazo zinaleta hofu au hata kusababisha  kuto kumuamini mtu kabisa, sababu tu unawaza vitu sivyo na ukasababisha matatizo lakini badala yake unaweza tumia mawazo yako kuwaza vitu chanya juu ya mapenzi yenu na usiingie katika matatizo.

Rabiadamary (mmasaimfupi)

Huyu muigizaji wa Afrika kusini ala shavu kwenye Fast and Furious 8

$
0
0

Muigizaji wa Afrika kusini, Charlize Theron ametangazwa kuwa mmoja wa waigizaji wa filamu mpya ya Fast and Furious 8.

vin-diesel

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 48, ameungana na  Vin Diesel, Jordana Brewster,Tyrese Gibson, Jason Statham, Chris ‘Ludacris’ Bridges na wengine kwenye filamu hiyo ambayo itatoka April 17, 2017.

Charlize Theron ni staa wa filamu kama  Mad Max: Fury Road (2015),  A Million Ways to Die in the West (2014),  The Italian Job (2003) na zingine nyingi, Pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar.

 

PICHA:Mwanamke huyu ameamua kuacha kazi ili apate muda wa kumnyonyesha mpenzi wake mwenye umri wa miaka 36.

$
0
0

  EXCLUSIVELY..!! Mwanamke mmoja jijini Atlanta nchini Marekani,Jenipher Mulford  ameamua kuacha kazi ili apate muda wa kutosha kumnyonyesha mpenzi wake Brad Leeson mwenye umri wa miaka 36 ambae ni mkufunzi wa mazoezi ya viungo.

shidaaaaa 0001                                        Jenipher Mulford na mpenzi wake Brad Leeson.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la The Sun Mwanamke huyo amekiri kuwa kwa muda mrefu alitamani kuanza mahusiano ya kimapenzi kwa mtindo wa kunyonyesha (Adult Breastfeeding Relationship),baada ya kusoma baadhi ya vitabu vinavyodai kuwa mahusiano ya aina hiyo huwafanya wapenzi kupendana na kudumu kwenye mahusiano yao na kuongeza kuwa licha ya kujaribu mara kadhaa kumtafuta mwenza atakaeridhia mahusiano ya aina hiyo mitandaoni bila mafanikio,hatimae aliamua kumtafuta aliekua rafiki yake enzi za utoto (Brand Leeson) ambae aliridhia wazo hilo ambapo mwanaume huyo hunyonya maziwa hayo kwa mrija maalumu au kwa mdomo kama mtoto mchanga.

shidaaaa milk pipe

shidaaaa 0002  “We both wanted the same thing out of the relationship – a magical bond that only breastfeeding an achieve.When I read about the pure joy it brought others, I was desperate to seek out a partner to share an emotional bond with….We both wanted the same thing out of the relationship – a magical bond that only breastfeeding an achieve”.Alidai Mwanamke huyo.

Jen has to be suckled every two hours as the pair attempt to get her milk flowingJenipher ambae ni mama wa binti mwenye umri wa miaka 20,amedai kuwa licha kutonyonyesha kwa muda mrefu sasa,kila baada ya msaa mawili huyatingisha matiti yake na kuvuta hisia kwa kujifikirisha kuwa ana mtoto anaehitaji kunyonya ikiwa ni pamoja na kumeza vidonge “flax seed” sambamba na mlo maalum ambao husaidia mwili wake kuzalisha maziwa ya kutosha yanayofanya mpenzi wake ambae ni mkufunzi wa mazoezi ya viungo kuwa na mwili wenye nguvu na kufanya mahusiano yao kuwa imara siku zote.

Brad loves a workout at the gym and believes the milk will help him keep fit

JE KUNA FAIDA ZA MAZIWA YA BINADAMU KWA WATU WANAOFANYA MAZOEZI…?

1.Kikombe kimoja cha maziwa ya mwanadamu (mwanamke) huwa na kalori 170,gram 10 za wanga na gram 2 za protini.

2.Kama wengi wetu tujuavyo,maziwa hasa ya mama kwa mtoto husaidia ukuaji wa mtoto,hivyo baadhi watu wanaofanya mazoezi kama ya kunyanyua vitu vizito wanadaiwa kutumia sababu hiyo kama kigezo cha kutafuta maziwa ya binadamu(mwanamke) kwa aliji ya ukuaji wa misuli na miili yao kwa ujumla.Chanzo-: Men’s Health

NOTE :Hata hivyo hakuna utafiti rasmi unaokubali au kukataa faida hizi za maziwa ya binadamu (mwanamke)kwa watu wanaofanya mazoezi ya viungo hivyo suala hili libaki kuwa maamuzi ya watu binafsi kati ya anaenyonya na anaenyonyeshwa japo kwenye jamii za watu wetu kitendo kinaweza kutafsiriwa kama ukosefu wa maadili au udhalilishaji.

 

 

Dudu Baya: Sina Imani na wasanii waliopo chini ya label za Bongo, wakishapata umaarufu wanageuka menejimenti zao

$
0
0

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu baya ametoa maoni yake kuhusiana ongezeko la label za muziki Bongo, ambapo amesema ni jambo zuri ila tatizo wasanii wanaosimamiwa na label hizo.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha Ea Radio, Dudubaya amesema wasanii wengi wa bongo wanaingia mikataba wasiyoridhika nayo ili kupata umaarufu na baadaye wakishafanikiwa wanaanza kuongea maneno machafu kuhusu menejimenti zilizowatoa.

Dudu-Baya

Ametoa mifano ya Bongo Records enzi Wateule, Dogo janja alivyoondoka TipTop na kuanza kusema hakuwahi kulipwa chochote pamoja na mifano mingi ya watu waliojaribu kuanzisha lebel wakaishia njiani.

Ametolea mifano lebel kama WCB na nyinginezo ambapo ameisema inafanya vizuri lakini haamini kabisa wasanii wake endapo watadumu.

 

Rich Mavoko adai kuwa kuna msanii mkubwa wa Bongo alimuambia asisaini WCB

$
0
0

Sio watu wote waliofurahia Rich Mavoko kusainiwa chini ya label ya WCB, ikiwemo wasanii wengine wakubwa wa Bongo Fleva.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, Mavoko amedai kuwa kuna msanii alimkataza kusainiwa chini ya label hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz baada ya taarifa za yeye kusainiwa kwenye label hiyo kutoka.

wasafi (1)

“Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz ” Mavoko alifunguka. “Kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu.”

Rich Mavoko tayari ameachia wimbo wa kwanza akiwa chini ya label hiyo, Ibaki Story

Abdu Kiba afafanua kauli yake ya kuwa yupo tayari kufanya kazi chini ya label ya WCB, asema watu hawakumuelewa vizuri

$
0
0

Msanii wa Bongo Fleva, Abdu Kiba amefafanua kauli yake aliyoitoa kwenye kipindi cha Planet Bongo kuwa yupo tayari kufanya kazi na label ya WCB iwapo watakubaliana.

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” Chid Benz alifunguka kwenye kipindi icho.

Abdul

Abdu kiba ameibuka kuifafanua kauli hiyo ambapo amedai kuwa watu walimuelewa vibaya lakini hakuwa na maana hiyo,

“Mimi nina label yangu, nina label inayosimamia kazi zangu, inasimamia muziki wangu, Inasimamia kila kitu changu” Abdu Kiba ameiambia AyoTv  “Nashangaa taarifa ambazo zinanifika tofauti, kutoka kwa mashabiki, kutoka kwenye blogs tofauti like kwamba Abdu Kiba anasema anaweza kukaa mezani na kusaini sijui label sijui ya nini nini No, siwezi kufanya hivyo kwasababu nina label yangu, Ila labda wakati naongea lile neno watu walinielewa tofauti” Abdu Kiba alifafanua.

Abdu Kiba amesema yeye yupo tayari kushirikiana kwenye kazi tu lakini sio kuama label.

Video: Utavunjika mbavu ukiona jinsi Kevin hart anavyofanya ‘shopping’ ya viatu

$
0
0

Mbali ya uchekeshaji Kevin Hart ni mpenzi mkubwa viatu ‘Snekaer’ na tayari amesaini dili la mamilion na kampuni ya Nike kutengeneza viatu vyake.

Complex huwa wana utaratibu wa kufanya Shopping ya viatu na Mastaa wakubwa na sasa ni zamu ya Kevin Hart, Tazama hapo juu!


Ronaldo aongoza orodha ya wanamichezo matajiri duniani, LeBron James na Kevin Durant nao wapo

$
0
0

Jarida la Forbes limetoa orodha ya wanamichezo 10 Matajiri zaidi duniani na Mwanasoka nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameongoza orodha hiyo akiwa na utajiri wa dola milioni 88 ambazo ni zaidi ya bilioni 190 za kitanzania.

Nafasi ya pili imeshikiliwa na mpinzani wake mkubwa kwenye mpira wa miguu, Lionel Messi ambaye na utajiri wa dola milioni 81.4 ambazo ni zaidi ya bilioni 178 za kitanzania.

top-10

Dola milioni 32 ambazo ni zaidi ya bilioni 70 za kitanzania katika utajiri wa Ronaldo unatokana zaidi na mikataba ya matangazo kupitia account zake za mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram na Facebook.

Wengine ni pamoja na:

3. LeBron James
Total Earnings: $77.2 million

4. Roger Federer
Total Earnings: $67.8 millio

5. Kevin Durant
Total Earnings: $56.2 million

6. Novak Djokovic
Total Earnings: $55.8 million

7. Cam Newton
Total Earnings: $53.1 million

8. Phil Mickelson
Total Earnings: $52.9 million

9. Jordan Spieth
Total Earnings: $52.8 million

10. Kobe Bryant
Total Earnings: $50 million

Hupendi kutumia Sukari? Zijue faida za asali kwenye mwili wako

$
0
0

Kwa miaka mingi asali imetumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali, ila najua wengi wetu tunajua tu kuipaka pale tunapo ungua na moto ila kuna faida zingine nyingi za asali wengi wetu hatuzijui au tu hatujaamua kujua faida zake.

Kama sukari ni tatizo kuipata unaweza ukafanya asali kama ndo sukari katika chai yako, achilia mbali utamu unaopatikana katika asali lakini pia asali ni dawa, unaweza itumia asali katika vitu tofauti tofauti, kwenye mkate, keki na vingine vingi.

asali

Faida za Asali Mwilini

Asali inasaidia kuchochea kumbukumbu kwa wale walio na matatizo ya kusahau sahau asali inasaidia sana kukufanya ukumbuke, Tunaweza kusema ina boost Kumbukumbu zako.

Matatizo ya kupata usingizi yanaweza kutibika kwa kutumia asali mara kwa mara, na inaweza kusaidia watu wanaopata matatizo ya usingizi na walale vizuri,asali pia ni dawa ya mba kichwani unaweza kuchanganya na maji ya moto na kupaka katika sehemu husika na kuiacha kwa muda kabla haujaiosha.

kwa wanawake wanaopenda urembo,Asali pia unaweza kuipaka usoni kwa muda na ukaitoa na kunawa na maji ya uvugu uvugu husaidia kun’garisha ngozi na kuifanya ngozi yako iwe na mvuto. kama unataka kutoka na unahisi uso wako haujakaa vizuri paka asali osha alafu paka vipodozi na utaonekana mrembo sana.

Nimeona watu wengi wakiangaika kupunguza matumbo na uzito kwa kutumia madawa, ambayo kiukweli hakuna anaejua Madhara yake baadae kwani madhara huwa hayaonekani kwa muda mfupi, wakati mwingine madhara huchukua miaka kuonekana,

Lakini  Asali, Ndimu na Maji ya Moto, inaweza saidia vitu vingi japokuwa baadhi ya watu wanadhani asali na ndimu ni sumu. Ila si kweli? Asali ukiiweka kwenye maji ya moto na kukamulia kipande cha ndimu ni dawa ya vitu vingi.

asa

kama Mmen’genyo wa chakula chako,Ukiwa unatumia Asali maji ya moto na ndimu, itasaidia (digestion ) mmen’genyo wako wa chakula utafanyika haraka zaidi na kukusaidia kutoka kuwa na kitambi,pia husaidia kupata choo kwa wale wanaopata tabu kupata choo.

Asali pia ni dawa ya mafua na Kikohozi,Kama una mafua na kifua cha kubana sana, tumia asali na maji ya moto kamulia ndimu, itakusaidia kufanya upumue vizuri.Tumia mara mbili au tatu kwa siku na utaona maajabu.

Asali pia husaidia Kutoa Sumu Mwilini na Mafuta,Wakati unaangaika kutafuta Dawa za kutoa sumu mwilini, tumia mchanganyiko huo, utashangaa unaenda sana chooni, kiukweli unaweza kuharisha sana kipindi cha mwanzo ukahisi unaumwa ila ndo jinsi uchafu au mafuta ya mwili wako yatakavyotoka mwilini, lazima uharishe, kwahiyo usishangae kupata safari nyingi za chooni.

 

Picha: Beyonce ashitakiwa kwa kuiga vipande vya filamu na kutumia kwenye ‘Lemonade’

$
0
0

Beyonce amebuluzwa Kortin kwa madai ya kukopi vipande vya Trailer ya album yake ya ‘Lemonade’ iliyooneshwa HBO.

Kwa mujibu wa Hollywood Reporter, muandaji wa filamu  Matthew Fulks amemshitaki Beyonce kwa madai ya kukopi filamu yake fupi “Palinoia” na kutumia kwenye Trailer ya ‘Lemonade’, Kwenye madai hayo Fulks amedai kuwa mwanadada huyo amekopi zaidi ya vipande tisa kutoka kwenye filamu yake hiyo.

B1_o8hd8d

B2_o8hd8w

B3_o8hd9s

 

B4_o8hdac

B5_o8hday

B6_o8hdbc

B7_o8hdbs

B9_o8hdcv

B8_o8hdce

 

NEW VIDEO:”Company”,Justin Bieber.

$
0
0

Company“…!! hili ni jina la video mpya ya Justin Bieber  inayopatikana kwenye album yake ya nne inayofahamika kama Purpose  iliyotoka mwaka 2015,single hii imeandikwa na Bieber mwenyewe,Jason Boyd,James Abrahart,Andreas Schuller na Thomas Troelsen,wimbo ambao umejumuisha vionjo vya mahadhi ya “electro-pop” na R&B huku gitaa likisikika kwa mbali pia.

bieberrrrrr on stage 09Mashairi ya wimbo huu yanaelezea simulizi ya mapenzi ya mtu ambae yupo kwenye mahusiano ila bado hajamfahamu vyema mwezi wake…..sitaki nikumalizie uhondo enjoy.

 

MASTER JAY:”Nimekua kwenye mahusiano na Shaa kwa miaka 10,kabla ya watu kujua”.

$
0
0

Mtayarishaji nguli wa muziki wa Bongofleva,na mmiliki wa record label ya MJ Records, Joachim Kimario “Master Jay” amedai kuwa alikua kwenye mapenzi ya siri na Mwanamuziki Sara Kaisi “Shaa”kwa muda wa miaka kumi kabla ya mahusiano yao kuwa hadharani.

Kwenye  mahojiano aliyofanya na gazeti la   MTANZANIA hivi karibuni, Master Jay alisema walikuwa katika mapenzi ya siri kwa muda wote huo hadi walipoamua kuweka wazi baada ya kuona watu wengi wakihoji ukaribu wao.
master jay and shaaa 0007“Nilimpenda Shaa kwa sababu ni msichana anayejielewa pamoja na kazi zake anazozifanya ni nzuri, hata hivyo tumeendana katika mapenzi yetu,’’ alidai Master Jay ambae ana watoto watatu aliozaa na mke wake,ila mpaka sasa hana mtoto na  Shaa.

Master jay na watoto wake...                                           Master Jay akiwa na watoto wake.

Viewing all 2148 articles
Browse latest View live